SMAUJATA ni jumuiya ya kijamii ambayo imesajiliwa chini ya sheria ya asasi za kiraia (CAP .337 RE 2022) kwa usajili namba S.A.23969, SMAUJATA ilianzishwa na shujaa Sospeter Mosewe Bulugu mwaka 2022 kwa lengo la kuchochea mabadiliko chanya na kuleta maendeleo endelevu kijamii na kiuchumi.